October 3, 2017



Pamoja na kuwa amefunga mabao mawili, Ibrahim Ajib wa Yanga ndiye mchezaji anayeogopwa zaidi kwa kipindi hiki katika kikosi cha Yanga.

Hii ni baada ya timu za Ligi Kuu Bara kuwa zimecheza mechi 5 kila moja.

Ajib anaonekana kuwa tishio zaidi kwa mabeki wa timu pinzani kutokana na namna ambavyo amekuwa akicheza.

Katika kikosi cha Yanga, Ajib ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Simba, anaonekana ndiye mchezaji bora zaidi na tishio kwa kila timu inayokutana na Yanga.

Utaona, ndani ya kikosi cha Yanga, Ajib anaonekana na mchango mkubwa zaidi na tishio kutokana na anavyocheza akijiamini.


Mabao yake mawili, yameipa Yanga pointi sita kutoka kwa Njombe Mji pamoja na Ndanda FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic