October 27, 2017




Promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA imeanza kwa kishindo cha hali ya juu ambapo wateja wa kampuni hiyo ambayo ni wadhamini wa klabu za Simba, Yanga na Singida United wanapata fursa ya kujishindia pikipiki ya miguu mitatu aina ya TVS KING mpya huku zawadi nyingine zikiwa ni tiketi tatu za kwenda nchini Uingereza kushuhudia mechi ya EPL mubashara na jezi orijino zitakazokuwa zikitolewa kila wiki.

SportPesa ilizindua promosheni hiyo siku ya Jumatano ya Oktoba 25 kwenye uwanja wa Bakhresa Manzese jijini Dar es Salaam majira ya saa tano kamili asubuhi ambapo jumla ya TVS KING 100 zitatolewa huku mshindi mmoja akijiondokea na TVS KING yake mpya kila siku kwa siku 100.

Kama ilivyo kwamba kila mshindi mmoja anajiondokea na TVS KING mpya kila siku, tayari mshindi wa kwanza ameshapatikana katika droo iliyofanyika siku ya Alhamisi ya Oktoba 26 ambayo ilirushwa na kituo cha televisheni cha Clouds majira ya saa 1:20 usiku kabla ya taarifa ya habari.
Deus Benedicto Ninalwo, mwenye umri wa miaka 30 ndiye alifungua pazia la ushindi wa TVS KING kwenye droo hiyo ya kwanza.

Furaha ya ushindi
Deus ambaye ni mwalimu wa shule ya Sekondari Mbugun iliyopo Halmashauri ya Meru jijini Arusha, alitusimulia kwa ufupi jakamoyo lililomkumba baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa TVS KING kati ya zile 100 zinazoshindaniwa.

“Nilitoka kazini kwasababu nilikuwa najisikia vibaya, nikawa nimelala ndani ndio nikapigiwa simu nikaambiwa nimeshinda TVS KING ilikuwa mida ya saa kumi jioni kwakweli nilipona ghafla licha ya kutomeza dawa.

“Kwanza nilikata simu kwasababu sikuamini nilichokisikia na mtu wa SportPesa akapiga tena, nilihisi kama ni matapeli lakini alivyonifanyia mahojiano akataka majina yangu matatu, namba ya kitambulisho changu na TIN namba yangu, kwahiyo alivyotaka TIN namba yangu sasa hapo ndio nikaanza kuamini kuwa nimeshinda.

“Nilipomwambia mwenzangu kuwa nimeshinda TVS KING kutoka SportPesa, kwanza akaniambia nikae kimya nisimwambie mtu yoyote mpaka nitakapoiona, na nikiambiwa kutuma hela nisitume huenda ni matapeli lakini mpaka kufikia sasa nimeamini kuwa nimeshinda.

Utofauti wa SportPesa
Bwana Deus ambaye amekuwa akicheza na SportPesa kwa wiki kadhaa sasa alikwenda mbali zaidi na kueleza kiilichomvutia kucheza na SportPesa.
“Nina wiki mbili tangu nimeanza kucheza na SportPesa na kitu kikubwa kilichonivutia kwanza dau lao la Jackpot ni kubwa (TZS 211, 868, 120/= wiki hii), na odds zao ni nyingi na kitu kingine ni kuwa pesa yako unapewa palepale baada ya ushindi. Juzi nilicheza na mechi za juzi zikaishia jana na usiku wa saa kumi huo huo nikapata hela yangu.
Ushauri wa bure
Bwana Deus alimalizia kwa kuwashauri vijana wenzie na watanzania kwa ujumla kuchangamkia fursa ya TVS KING ambayo inatolewa na SportPesa huku akielezea matumizi ya TVS KING yake hiyo mpya.
“Kushinda inawezekana, kushiriki ndio kushinda, mimi nisingeshiriki nisingeweza kushinda kwahiyo vijana wenzangu tushiriki kwasababu hii itatutoa kimaisha na nimefurahi kwasababu nimeshinda.
“TVS KING hii niliyoshinda nitamuweka mtu atakuwa ananifanyia kazi ili niweze kujiingizia kipato zaidi ya kazi yangu ya ualimu,” alisisitiza Bwana Deus.
Jinsi ya kushiriki 
Ili kushiriki kwenye promosheni hii ya SHINDA TVS KING NA SPORTPESA, kwanza kabisa unatakiwa kujisajili kwa kutuma neno GAME kwenda 15888 (kama bado hujajisajili), weka pesa kwa namba ya biashara 150888 kisha piga *150*87# au tembelea www.sportpesa.co.tz kuweka utabiri wako mara nyingi.


Ukishaweka utabiri wako, utatumiwa ujumbe unaokutaka kutuma neno SHINDA kwenda 15888 ili kuingia kwenye droo. Kadri unavyozidi kucheza mara nyingi ndivyo unajiongezea nafasi ya kushinda kila siku.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic