October 8, 2017


Yanga imetoka sare ya bila kufunga na KMC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Yanga na KMC zimekutaka katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complec, Chamazi, usiku huu.
Ilikuwa ni mechi ya vuta nikuvute na KMC inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Fred Felix Minziro inaonekana ilipania kushinda mechi hiyo.

Hata hivyo, Yanga ilipumzisha nyota wake wengi wakiwemo wale waliokuwa majeruhi na kutoa nafasi kwa wale ambao hawajapata sana nafasi katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Baada ya mechi hiyo, Minziro alisema walitaka kushinda pamoja na kwamba ni sehemu ya mechi zao za maandalizi.

Minziro amesema ushindi ingekuwa ni sehemu ya kujaza morali, lakini sare pia ni sehemu ya kuonyesha wanaweza kucheza kwa ushindani na watautumia mchezo huo kama sehemu ya mafunzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic