October 8, 2017




Mmoja wa mshambulizi mwenye kasi wa Yanga, Said Maulid maarufu kama SMG amesema wachezaji wakongwe ambao wana nafasi ya kusaidia vijana wafanye hivyo.

SMG amesema ni vizuri kuendelea kizazi cha soka kwa kuwa watoto na vijana wengi wanapenda kucheza.

“Mimi ninaishi Mbagala, lakini sikai ndani tu. Ninapopata nafasi nakwenda jirani kuna vijana wanacheza mpira nawasaidia.

"Si lazima kutoa fedha, hata unapowaita na kuwahamasisha ni jambo jema sana,” alisema.

SMG ambaye baada ya kuondoka Yanga alikwenda nchini Angola na kujiunga na Bravo de Marquize ya Angola amesema ataendelea kusaidia vijana.


“Hata mimi nilisaidiwa, hivyo ni lazima niwasaidie vijana wengine,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic