October 29, 2017


Beki wawili, Kelvin Yondani wa Yanga na kiungo mkabaji wa Simba, James Kotei ndiyo waliomaliza mjadala mkubwa wa mechi ya watani kuhusiana na wakali Ibrahim Ajibu na Emmanuel Okwi.

Simba na Yanga zilimaliza ubishi kwa sare ya bao 1-1 katika mechi iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Okwi na Ajibu walikuwa mjadala mkubwa na ilionekana ni kama mechi yao kwa kuwa ndiyo walikuwa tegemeo kubwa la watani hao.



Yondani alionekana kuwa alipewa kazi ya kumdhibiti Okwi ambaye alipambana naye kila mara na mara chache alisaidiwa na Andrew Vicent 'Dante'.

Kwa upande wa Simba kwa kuwa Ajibu alikuwa akitembea sana, alikuwa na kazi ya kumtuliza Ajibu asifanye "yale mambo yake".

Mechi hiyo ilionekana ni ngumu kwa kila upande na Okwi na Ajibu hawakufanikiwa kufanya yale makeke ambayo yamezoeleka.

Ingawa wote wawili walianzisha "move" zilizozaa mabao yote mawili yaliyotengeneza sare ya bao 1-1, lakini hakuna aliyefunga au kutamba unaweza kusema alikuwa ni nyota wa mchezo kutokana na kazi nzuri ya wawili hao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic