October 8, 2017


Baada ya mapumziko, kikosi cha Simba kitarejea mazoezini kesho kuanza kujiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba ilikuwa katika mapumziko baada ya mechi dhidi ya Stand United ambayo ilishinda kwa mabao 2-1 na kukwea kileleni mwa Ligi Kuu Bara.

Simba itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa jijini Dar es Salaam na imeelezwa mazoezi hayo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo katika uwanja huo.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wanaanza kujiandaa dhidi ya Mtibwa Sugar wanaoonekana kuwa na mwendo mzuri katika ligi hiyo.


Mtibwa Sugar ni kati ya timu ambazo hazijapoteza mchezo hadi zinafikisha mechi tano na tayari imejikusanyia pointi 11 sawa na Simba ikwia katika nafasi ya pili. Hii inafanya matazamio kuwa mechi hiyo itakuwa ngumu kwa kila timu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic