October 8, 2017




Na Gharib Mzinga
Ndanda FC imeendelea kucheza mechi za kirafiki katika ukanda wake wakati Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kutokana na kalenda za mechi za Fifa.

Jana Jumamosi, kulikua na mchezo wa kirafiki kati ya Ndanda FC imeitwanga East Coast FC inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa.

East Coast inatokea mkoani Lindi, imekutana na kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Ndanda FC.
Ndanda FC ilianza kupata bao lake katika dakika ya 2 kupitia Jacob Massawe na Salum Mineli akaongeza la pili.
Huku ikionekana kama East Coast wanaweza kusawazisha, Massawe tena akaongeza bao la pili na Ndanda wakaenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao hayo matatu.

Kipindi cha pili mwanzoni kilionekana ni kizuri kwa East Coast lakini Ndanda wakageuza mambo na kufunga bao la nne katika dakika ya 57 kupitia Emsi Tiba.
East Coast walionekana kuwa wabishi hadi walipopata bao la “kuchafua gazeti” katika dakika ya 70 mfungaji akiwa ni Abdallah Rihame.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic