October 6, 2017


Pamoja na kuwapumzisha washambuliaji wake wawili, Donald Ngoma na Obrey Chirwa kutokana na kuwa majeruhi. Yanga imempumzisha kiungo mkongwe, Thabani Kamusoko.


Kamusoko naye alikuwa majeruhi na ataanza mazoezi rasmi Jumatatu kama ilivyo kwa wengine.

Leo, Kamusoko raia wa Zimbabwe alionekana akiwa mazoezini pamoja na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa Uhuru lakini hakushiriki mazoezini.

Kwa upande wa Washambuliaji hao wawili raia wa Zambia wamekuwa wakiandamwa na majeruhi na taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, daktari ameamua kuwapumizisha.

Suala la majeruhi au kadi, nalo limekuwa ni sehemu ambayo inamtatiza Kocha George Lwandamina ambaye msimu uliopita ndiye aliyeiwezesha timu hiyo kubeba ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic