October 5, 2017



Kikosi cha Simba kimewasili jijini Dar es Salaam baada ya mechi za mikoani.

Wachezaji wa Simba wamepewa mapumziko ya siku tatu kabla ya kurejea kazini.

Simba ilikuwa Kanda ya Ziwa kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC na baadaye Stand United na imefanikiwa kuvuna pointi nne.

Lakini ilicheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Milambo ya Tabora na Dodoma FC na kufanikiwa kupata sare na kushinda moja.

Simba imewasili jijini Dar es Salaam leo mchana na wachezaji wake watapumzika hadi hapo watakapoanza mazoezi Jumapili.


Baadhi ya wachezaji, wako katika kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars inayojiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi kwenye jijini Dar, Jumamosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic