October 5, 2017



Kikosi cha Taifa Stars chini ya Kocha Salum Mayanga kimefanya mazoezi muda mfupi tu na kurejea hotelini.

Stars imefanya mazoezi hayo kwa muda mfupi kwenye Uwanja wa Boko Veterani Dar es Salaam, leo asubuhi.

Wakati wengi walitarajia ingejifua kwa muda mrefu, lakini ndani ya saa moja kila kitu kilikuwa kimekamilika na timu imeondoka eneo hilo.

Hata hivyo, imeelezwa Stars itaendelea kujifua leo jioni kwenye uwanja huo.


Timu hiyo ya taifa ya Tanzania inajiandaa kuivaa Malawi katika mechi ya kalenda ya Fifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic