October 6, 2017



Kikosi cha taifa Stars kinatarajia kufanya mazoezi yake ya mwisho leo kabla ya kuivaa Malawi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Taarifa za awali zilieleza Stars itajifua kwenye Uwanja wa Boko Vetarani lakini baadaye ilielezwa lazima wafanye kwenye Uwanja wa Uhuru kwa kuwa ndiyo watakaochezea mechi na wanapaswa kuzitumia angalau mara moja, nyasi bandia.


Stars itaongozwa na nahodha wake, Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji lakini wako baadhi ya wachezaji kutoka nje ya Tanzania kama Saimon Msuva na Abdi Banda ambao watashirikiana na wachezaji wanaocheza katika ligi ya nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic