October 28, 2017

MSHINDI WA KWANZA WA SHINDANO LA VIPAJI VYA SAUTI AKIKABIDHIWA ZAWADI YAKE YA RUNINGA.
Washindi 10 wa Shindano la Vipaji vya Sauti wamepatikana katika shindano la kuvutia lenye ushindani wa juu lililomalizika hivi punde jijini Dar es Salaam.

Washindi 10 wamepatikana na watapata nafasi ya kufanya kazi chini ya Startimes Ltd huko jijini Beijing China.

Washindi hao wamepatikana katika ushindani mkali mbele ya majaji watatu wakiongozwa na JB na Mrisho Mpoto.

Haikuwa kazi rahisi kwa majaji na washiriki wenyewe kutokana na ushindani mkali uliojitokeza.

Mmoja wa waigizaji maarufu nchini, Muhogo Mchungu alijikuta akiangukia pua baada ya kuzidiwa ujuzi na vijana.

Washiriki 25, watano kutoka Mwanza, watano kutoka Zanzibar na 15 wa Dar es Salaam, walichuana vikali kupata washindi 10 wanaokwenda kufanya kazi nchini China.


















0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic