October 26, 2017


Yanga imeanza kupoteza matumaini ya kumpata kiungo wake nyota Thabani Kamusoko raia wa Zimbabwe.

Kamusoko ambaye alikuwa majeruhi na kupumzisha bado inaonekana hayuko katika kiwango sahihi.

“Kamusoko bado hajawa vizuri, ukweli sidhani kama ataweza kucheza dhidi ya Simba,” kilieleza chanzo.

“Kocha alikuwa anamhitaji sana lakini namna hali ilivyo, sidhani.”

Taarifa zinaeleza, Kocha George Lwandamina kama ameona hali ilivyo na ameanza maandalizi ya kucheza bila Kamusoko.

"Kweli kocha ameona haiwezekani na ameanza kujiandaa kivingine," kilifafanua chanzo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic