November 7, 2017




Uongozi wa klabu ya Azam FC imeamua kuvunja mkataba na mshambulizi wake, Yahaya Mohammed raia wa Ghana.

Azam imeona Mohammed ameshindwa kuonyesha kile walichokitarajia hivyo kuamua kumpa nafasi aende zake na inaonekana nafasi hiyo wataitumia kusajili mshambuliaji mwingine.

Siku nne zilizopita, Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioba alisema anahitaji washambuliaji wengine wawili ili kuongeza nguvu ya kikosi chake.

Huenda ndiyo utaratibu umeanza ili kuhakikisha Azam FC inajiweka sawa kwa ajili ya mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara baada ya dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa katikati ya mwenzi huu.



Azam imefikia uamuzi wa kuvunja mkataba na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 baada ya kuonesha kiwango duni tofauti na matarajio yao walipomchukua mwaka jana wakati wa dirisha Dogo la usajili.

"Nichukue nafasi hii kuwafahamisha kwamba hatutaendelea kuwa naye, uongozi umekutana naye, wamezungumza kuhusiana na suala lake na wamemalizana. Hivi sasa Mohamed sio mchezaji tena wa Azam FC baada ya makubaliano kati yake na uongozi," alisema Jaffary Idd, Msemaji wa Azam FC.

Maganga amesema tayari wameshampatia release letter na pamoja na hayo tayari wameshampatia kila kitu ikiwemo tiketi ya ndege ambapo wanatarajia ataondoka kurudi kwao Ghana Jumanne hii.

"Tutamkumbuka Yahaya, kwa Maana kwamba yale ambayo ameyafanya kwenye timu yetu, ametusaidia kupata ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na pia msimu ndiye aliyefunga bao la kwanza," amesema.

Mbadala wa Yahaya Mohamed kwa mujibu wa Afisa Habari Jaffary Maganga, ni kwamba atatangazwa baada ya benchi la ufundi kufanya tasmini na kuchambua wale wanaowahitaji.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Azam akitokea Aduana Stars ya Ghana, ambayo aliisaidia kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Ghana msimu 2015/16, Mohammed pia aliiibuka mfungaji bora namba mbili wa ligi hiyo kwa mabao 15 aliyofunga nyuma ya Latif Blessing wa Liberty Proffesional aliyetupia 17.



Mohammed alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika mwaka juzi nchini Afrika Kusini na timu hiyo kuwa washindi wa pili.

Wakati anaanza, alionyesha cheche zake lakini baadaye alionekana kushindwa kufanya vema kama ambavyo wengi walitarajia afanye.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic