November 7, 2017




Mshambuliaji Donald Ngoma, ameendelea na matibabu kwao Zimbabwe na imeelezwa anaweza kurejea nchini wiki hii, kuendelea kujifua.

Ngoma ameendelea na matibabu na kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa Yanga amesema, Ngoma amtarejea wiki hii na kuanza mazoezi ya taratibu.

"Yuko Zimbabwe kama ulivyosikia, aliomba ruhusa ya kwenda kutibiwa kwao. Ila sasa anaendelea vizuri na atarejea wiki hii na kuanza mazoezi ya taratibu," kilieleza chanzo.

"Si Ngoma pekee, hata Kamusoko na Tambwe pia wanaweza kuanza mazoezi wiki. Matarajio yetu hadi wiki ijayo watakuwa wameungana na wenzao kikamilifu."

Tambwe raia wa Burundi na Kamusoko, nao wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic