Baada ya kukipumzisha kikosi chake kutokana na uchovu wa mechi dhidi ya Mbeya City na safari kurejea jijini DAr es Salaam, Simba inarejea mazoezini leo.
Simba inarejea katika mazoezi yake kujiandaa na mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Polisi, Kilwa, Dar es Salaam.
Kwa sasa Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 22, sawa na Azam FC ambao wana pointi kama hizo wakiwa katika nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment