November 21, 2017


Liverpool ina kibarua kigumu cha Ligi ya Mabingwa Ulaya pale watakaoivaa Sevilla ya Hispania, leo.

Lakini Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp, matumaini yake makubwa yako kwa mshambuliaji wake, Mohamed Salah.

Salah raia wa Misri anaonekana kuwa tegemeo kubwa la kufunga na kutengeneza mabao.

Katika mechi iliyopita alikuwa mwiba dhidi ya mabeki wa Southampton na kuisaidia Liverpool kushinda kwa mabao 3-0, yeye akifunga mawili katika mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha Klopp anaamini Salah akiwa katika kiwango kizuri atakuwa msaada mkubwa katika mechi hiyo ngumu dhidi ya Sevilla.







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic