Timu ya Beach Soccer ya Chuo cha Sayansi na Teknolojia (DIT) imeitwanga Lisbon kwa mabao 10-1 katika michuano ya vyuo iliyoanza leo kwenye Uwanja wa Escape One jijini Dar es Salaam.
DIT walionyesha kuwa na uhai zaidi kuliko Lisbon ambao walichoka mapema.
Mechi nyingine ambayo imechezwa leo ni Chuo cha Ardhi ambacho kimeibuka na ushindi wa mabao 5-4 dhidi ya Chuo cha Uandishi wa Habari cha DSJ.
Mechi hiyo ilikuwa kali zaidi kutokana na upinzani mkali kutokana na kila timu kuwa imara katika ulinzi lakini wepesi katika ushambulizi.
Gazeti namba moja la michezo nchini, lmedhamini michuano ya soka ya ufukweni ya vyuo.
Michuano hiyo inaendelea katika ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally ambao ni wachapishaji wa gazeti la Championi amesema lengo lao ni kusaidia michezo.
“Sisi tumejitokeza kuonyesha tunaunga mkono michezo. Lengo Kuu ni kusaidia na kuwasisitiza watu michezo ni muhimu kwa afya na ajira,” alisema.
Ally maarufu kama Jembe, amewaomba watu kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hiyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment