November 7, 2017


Mshambuliaji Olivier Giroud amezua hofu baada ya kuumia akiwa mazoezini katika timu ya taifa ya Ufaransa.

Giroud amekuwa akijifua na wenzake katika eneo la Clairefontaine kujiandaa na mechi dhidi ya Wales, Ijumaa.

Lakini alianguka na kushikilia mguu wake chini akionyesha kuwa na maumivu, mambo ambalo linaonyesha kuzua hofu kwa Arsenal.

Kocha Mkuu wa Ufaransa, Didier Deschamps amesema ni tatizo dogo na halitachukua muda mrefu.

Lakini mambo hilo limeonekana kutowafurahisha Arsenal ambao wanaonekana wanamhitaji kwa ajili ya michuano mbalimbali.


Mara kadhaa, kumekuwa na mgongano kati ya klabu na timu za taifa kuhusiana na wachezaji na kila upande umekuwa ukiona una haji ya kuwamiliki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic