November 27, 2017

Baada ya hivi karubuni kuwepo kwa taarifa kuwa timu za Simba na Yanga zinamwinda mfungaji wa Prisons ya jijini Mbeya, Mohammed Rashid ili ziweze kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo, sasa mambo huenda yakainyookea Yanga.

Hiyo ni kutokana na mchezaji huyo kudai kuwa anavutiwa zaidi na mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na anatamani sana siku moja kucheza naye katika timu moja.

Simba na Yanga zinamtaka Rashid mwenye miaka 22 na ambaye amekuwa akifunga katika viwanja vya mikoani.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Rashid ambaye kwa sasa ana mabao sita sawa na Mzambia wa Yanga, Obrey Chirwa ambao kwa pamoja wapo nyuma ya Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi mwenye mabao nane, alisema kuwa anavutiwa sana na aina ya uchezaji wa Ajibu, hivyo anatamani sana siku moja awe naye katika timu moja.

Alisema kwa sasa kama angekuwa naye timu moja basi angekuwa amefunga mabao mengi zaidi ya hayo aliyonayo hivi sasa kwa sababu anajua kupiga pasi za mwisho.

“Kusema kweli mchezaji ninayetamani sana siku moja niwe naye timu moja ni Ajibu, hii ni kutokana na aina ya uchezaji wake.

“Siyo mchoyo lakini pia anajua kupiga pasi za mwisho, hakika kama itatokea siku moja nikawa naye katika timu moja basi nitafunga sana,” alisema Rashid.

Hata hivyo, alipoulizwa kama yupo tayari kujiunga na Yanga hivi sasa, alisema: “Mimi sina tatizo kama watakubaliana na uongozi wangu Prisons kwa sababu bado nina mkataba nao.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic