Gattuso enzi zake akimvuruga kocha msaidizi wa Spurs. |
Klabu ya AC Milan ya Italia imetangaza kumfukuza kazi Kocha Vincenzo Montella kutokana na matokeo mabaya ambapo nafasi yake imetua kwa Gennaro Gattuso.
AC Milan ilipata droo dhidi ya Torino, jana Jumapili na kuiacha timu hiyo ikiwa katika nafasi ya saba, ikiwa nyuma kwa pointi 18 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya Italia ‘Serie A’, Napoli.
Milan imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu licha ya kufanya usajili wa gharama msimu huu na kuwaleta Leonardo Bonucci, Andre Silva and Hakan Calhanoglu kwa jumla ya paundi milioni 150.
Mwendo mbaya wa klabu hiyo katika mechi za ligi haujabadilika hata baada ya kuwekeza fedha nyingi majira ya joto ambako Leonardo Bonucci, Andre Silva na Hakan Calhanoglu walisajiliwa kwa gharama ya £150 milioni.
Vincenzo Montella |
Rossoneri hawajawahi kupitia kipindi kigumu kama hicho mwanzoni mwa msimu tangu 1941/42, ambapo walifungwa mara saba katika mechi 14.
Gattuso, kiungo wa zamani wa Milan ambaye alijulikana kwa utukutu na kucheza soka la kibabe, atachukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo baada ya kufundisha timu ya vijana, ambao wamepoteza mechi moja tu katika mechi tano walizocheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment