November 26, 2017


Bondia Mtanzania, Ibrahim Class Mgendera, jana usiku amefanikiwa kutetea taji la GBC uzito wa Light baada ya kumshinda kwa pointi Koos Sibiya wa Afrika Kusini.

Class alishinda kwa pointi za majaji wote baada ya kuonyesha kiwango kizuri kuanzia mwanzo wa pambano hilo lililofanyika Uwanja wa Uhuru.

Mwamuzi raia wa Ujerumani ndiye aliyesimamia pambano hilo, lililohudhuriwa na Waziri wa Habari Utamadunia Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Pambano hilo lilikuwa gumu kwa mabondia wote lakini dalili za Class kushinda zilianza kuonekana raundi ya nane baada ya kumjeruhi kwenye pua Sibiya ambaye alichafuka damu eneo hilo hadi mdomoni.

Baada ya hapo Class aliendelea kutawala pambano baada ya wawili hao kuonekana kupigana sawa katika raundi zilizotangulia.  

Class ambaye ana umri wa miaka 27 awali alitwaa taji hilo Julai 1, mwaka huu baada ya kumpiga Jose Luis Forero Atencio wa Panama kwa pointi Jijini Berlin, Ujerumani. 

Hilo linakuwa pambano lake la 21 kushinda kati ya 25 aliyocheza, akiwa amepoteza mapambano manne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic