FULL TIME
Mchezo umefikia tamati. Matokeo ni 1-1.
Dk ya 95: Muda wowote mchezo utamalizika.
Dk ya 93: Simba wanapambana kutafuta bao la ushindi lakini mambo ni magumu.
Dk ya 90: Zinaonyeshwa dakika 5 za nyongeza.
Dk ya 86: Simba wanafanya shambulizi kali, mpira unatoka nje, kipa wa Lipuli, Aghathoni anapewa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda.
Dk ya 81: Gyan anapiga shuti la moto, kipa anapangua inakuw akona.
Dk ya 78: Simba wanapata faulo nje ya eneo la 18.
Dk ya 77: Lipuli wanamtoa Karihe anaingia Waziri Ramadhani.
Dk ya 71: Simba wanamtoa Kotei anaingia Ally Shomari.
Dk ya 65: Anatoka Kazimoto anaingia Nichalaus Agey.
Dk ya 59: James Kotei wa Simba na Shaban Ada wanapewa kadi za njano kila mmoja kutokana na mchezo wa kibabe.
Dk ya 57: Seif Karihe anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Mlipili.
Dk ya 54: Niyonzima anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Laudit Mavugo.
Dk ya 50: Mchezo ni mgumu kwa timu zote.
Dk ya 47: Simba wameanza kwa kasi na wanaonyesha kutafuta bao la mapema.
Dk ya 45: Lipuli wanafanya mabadiliko, anatoka Hussein Rashid anaingia Kazila.
Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Dk ya 47: Mwamuzi anakalimisha kipindi cha kwanza. Matokeo ni 1-1.
Dk ya 45: Zinaongezwa dakika mbili za nyongeza.
Dk ya 45: Lipuli wanamiliki mpira kwa sekunde kadhaa.
Dk ya 38: Simba wanafika langoni mwa Lipuli lakini shuti la Haruna Niyonzima anapaisha mpira juu.
Dk ya 35: Novalty Lufunga wa Lipuli ameingia kuchukua nafasi ya Hamad Manzi.
Dk ya 32: Mchezo umepungua kasi, timu zimeanza kushambuliana kwa zamu.
Dk ya 24: Kasi ya mchezo sasa imebalansi kwa timu zote kumiliki mpira kwa zamu.
Asante Kwasi anaisawazishia Lipuli bao, anafunga kwa mpira wa faulo unaoingia wavuni moja kwa moja.
Dk ya 19: GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 17: Lipuli wanaanza kujipa vizuri.
Dk ya 15; Mwinyi Kazimoto anaipatia Simba bao la kwanza, alipata pasi kutoka Mzamiru. Akaubetua mpira kwa juu.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 10: Simba wanafanya shambulizi kali linalosababisha kona mbili mfululizo.
Dk ya 9: Kichuya anapiga shuti kali linapaa juu ya lango.
Dk ya 7: Simba wanamiliki mpira muda mwingi.
Dk ya 3: John Bocco anapiga shuti lingine linagonga nguzo.
Dk ya 2: Shiza Kichuya wa Simba anapiga shuti linagonga nguzo, kidogo mpira uingie ndani ya wavu.
Dk ya 1: Simba wameanza kwa kasi.
Mchezo umeanza.
Simba inaikaribisha Lipuli inayonolewa na Selamani Matola, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment