November 17, 2017



Kama ulivyosikia kuwa, uongozi wa klabu ya Singida United kumuondoa kikosini kiungo wake Deus Kaseke lakini pia kiungo anayechipukia kwa kasi, Kenny Ally.

Viungo hao wameondolewa kikosini kwa madai ya utovu wa nidhamu ingawa kuna taarifa walikuwa wakidai kutimiziwa mambo yaliyo katika mikataba yao ambayo Singida United hawakuwa wametimiza.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zimedai kuwa Kaseke na Ally waligoma kutoka katika nyumba walizokuwa wamepewa kukaa kwa muda ambazo walikuwa wametafutiwa wachezaji wa kimataifa wa timu hiyo waliokuwa wameenda kuzitumikia timu zao za taifa.

“Timu ilipokuwa Dodoma uongozi ulikuwa umewatafutia nyumba za kuishi wachezaji wote, baada ya kurudi hapa Singida pia ukafanya hivyo ambapo wachezaji wa kigeni walipewa vyumba vyao na wazawa pia walipewa vyumba vyao.

“Hivi karibuni baadhi ya wachezaji wa kimataifa walienda kuzitumikia timu zao za taifa ndipo Kaseke na Ken Ally wakaambiwa na uongozi wakute wanaishi katika vyumba ambavyo walikuwa wametafutiwa wachezaji hao wa kimataifa na watakaporudi itabidi wawapishe na wao warudi katika vyumba vyao walivyotafutiwa.

“Hata hivyo, baada ya wachezaji hao wa kimataifa kurudi, Kaseke na Ken Ally walipoambiwa wawapishe kwenye vyumba vyao wakagoma ndipo uongozi ulipokutana jana jioni (juzi) na ukaamua kuwatimua katika timu na leo hii (jana) wameondoka zao kwenda kwao Mbeya,” kilisema chanzo hicho cha habari.


Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahman Sima alisema: “Ni kweli tumewasimamisha kwa muda usiojulikana kutokana na kosa la utovu wa nidhamu na jana (juzi) mchana tumewakabidhi barua za kuwasimamisha,” alisema Sima. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic