November 2, 2017



Kikosi cha Singida United kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida kabla ya mechi ya keshokutwa Jumamosi.

Singida United watakuwa wenyeji wa Yanga katika mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Bara kwenye uwanja huo. 



Kesho itakuwa ni zamu ya Yanga kufanya mazoezi kwenye uwanja huo kabla ya mechi hiyo ya keshokutwa inayotazamiwa kuwa ngumu wakati Kocha wa Singida United, Hans van der Pluijm atakuwa anakutana na mwajiri wake wa zamani.

Mechi hiyo inawakutanisha Yanga dhidi ya Singida United na uongozi wa uwanja huo umekuwa ukisimamia zoezi la umwagiliziaji.

Uwanja huo, utatumika katika mechi hiyo ya kwanza lakini unaonekana hauna hali nzuri sana kama ambavyo wengi walitarajia baada ya matengenezo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic