November 27, 2017


Wakati dirisha dogo la usajili likiwa bado lipo wazi, kuna maamuzi yamefanyika ndani ya kikosi cha Yanga.

Mshambuliaji wa timu hiyo, Matheo Anthony, hivi karibuni aliamua kumfuata kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, akitaka kumpa ruhusa ya kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuchoka kukaa benchi.

Matheo aliyejiunga na Yanga akitokea KMKM ya Zanzibar, mara kwa mara amejikuta akikosa nafasi ya kutumika kwenye kikosi cha kwanza ambapo kwa sasa straika huyo amejiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes kwa ajili ya michuano ya Chalenji ambayo itaanza kutimua vumbi Desemba 3, nchini Kenya.

Chanzo kutoka Yanga kimeliambia Championi Jumatatu kuwa, mshambuliaji huyo alikuwa na kikao na Lwandamina akitaka amruhusu kuihama timu hiyo kwa sababu ya kukosa namba ambapo Kagera Sugar wamekuwa wakimtaka.

“Kweli kabisa hivi majuzi kocha Lwandamina aliongea na Matheo, kwa ajili ya kutaka aruhusiwe kwani amechoka suala la kukaa benchi.

“Na huenda kwenye dirisha hili la usajili anaweza kuondoka kwani Kagera Sugar wamekuwa wakimtaka kwa ajili ya kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi chao,” kilisema chanzo hicho.

Championi Jumamosi, lilimtafuta Matheo ambapo alisema: “Kweli nimeongea na kocha, Lwandamina kumuomba aniruhusu niondoke kwani nimechoka kukaa benchi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic