November 9, 2017



Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema wana nafasi ya kufanya vizuri katika mechi ya kirafiki dhidi ya Benini, Jumamosi.

Mayanga amesema watafanya vizuri pamoja na kuwa na pengo la nahodha wake, Mbwana Samatta.

Samatta ataikosa mechi hiyo kwa kuwa anatakiwa kupata matibabu kwa wiki sita baada ya kuumia goti akiichezea timu yake ya KRC Genk.

“Tumejiandaa vizuri na tuna nafasi ya kufanya vizuri, tutaimudu Benin,” alisema.


Kumekuwa na hofu kwa mashabiki wengi ambao wamekuwa wakilijadili suala la Stars kumkosa Samatta ambaye ndiye tegemeo katika ushambulizi kama kiongozi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic