November 9, 2017




Kikosi cha Yanga kitaendelea na mazoezi leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga inaendelea na mazoezi kujifua ili kukiweka kikosi chake sawa lakini kinakosa wachezaji takribani 10.

Wengi wa wachezaji hao ni wale waliochaguliwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachosafiri kwenda Benin kucheza mechi ya kirafiki wakati wa kalenda ya Fifa.

Lakini wachezaji watatu ambao wamechaguliwa katika kikosi cha timu ya vijana. Lakini kuna wachezaji wake nyota watatu Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko ambao ni majeuhi.

Hata hivyo, Yanga wamekuwa wakiendelea na mazoezi na wachezaji walionao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic