November 25, 2017


Mashambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi mwaka 2021 ambapo mkataba huyo mpya una maboresho mengi mazuri kwake.

Messi amesaini mkataba huo ambapo mshahara wake utakuwa ni pauni 500,000 (Sh bilioni 1.5) kwa wiki pamoja na dau la pauni milioni 80 ambalo amekabidhiwa kama fedha yake ya usajili mpya.
Kabla ya kusaini mkataba huo ilielezwa kuwa Messi anawaniwa kwa ukaribu na Manchester City na PSG.

 Katika mkataba huo, dau la timu nyingine kuweza kumsajili Messi limetajwa kuwa ni pauni milioni 626 (Sh trilioni 1.8).

Hadi sasa Messi ameichezea timu hiyo mechi 602na kufunga mabao 523 akishinda mataji 30 ikiwa ni tangu alipoanza kucheza timu ya wakubwa siku 4,788 zilizopita.

MATAJI YA MESSI

BARCELONA
La Liga (8): 2004-05, 2005-06, 2008-09, 2009-10, 2010-11, 2012-13, 2014-15, 2015-16

Copa del Rey (5): 2008-09, 2011-12, 2014-15, 2015-16, 2016-17

Champions League (4): 2005-06, 2008-09, 2010-11, 2014-15

TUZO BINAFSI
Ballon d'Or/FIFA Ballon d'Or (five): 2009, 2010, 2011, 2012, 2015

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic