Klabu ya Simba Imetoa tamko juu ya kiungo Said Ndemla ambaye kwa siku kadhaa alikuwa barani Ulaya nchini Sweden akifanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Ndemla ambaye anajulikana kwa kupiga mashuti ya mbali licha ya umbo lake kuonekana ni la wastani amekuwa kipenzi cha Wanasimba wengi kwa miaka kadhaa kutokana na kuonyesha uwezo mzuri hasa kwa kuwa amelelewa na timu hiyo.
Hii hapa ndiyo taarifa ya Simba:
Simba Sports Club
Dar es salaam
25-11-2017.
TAARIFA KWA UMMA
_____________________________
Mchezaji Said Hamis Juma (Ndemla) amefanikiwa kufuzu kwenye majaribio yake ya kucheza Soka la kulipwa barani Ulaya.
Ndemla aliyekuwa nchini Sweden kwa majaribio kwenye klabu ya Eskilstuna ya huko.anatarajiwa kurejea nchini siku ya jumatatu inayokuja.
Na mara baada ya kurejea. klabu za Simba na Eskilstuna zitaanza mazungumzo ya kimkataba ili kumwezesha kiungo huyo kwenda Sweden kwa ajili ya kucheza Soka huko.
Kiufupi klabu imefurahishwa na azma ya Ndemla ya kutaka kusonga mbele zaidi, na kama ilivyo desturi na utamaduni wa Simba, klabu haitasita kumruhusu mchezaji yoyote anayepata fursa adhimu kama hiyo itakayomsaidia mchezaji binafsi.klabu na Taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo kesho klabu ya Simba itakutana na viongozi wote wa matawi.
Mkutano huo ni maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa klabu wa tarehe 3-12-2017. na mkutano huo wa kesho utafanyika makao makuu ya klabu kuanzia saa Nne kamili asubuhi ya jumapili ya tarehe 26-11-2017.
Mwisho
Uongozi wenu unawaomba Wanachama na washabiki wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kesho uwanja wa Uhuru kuishangilia timu yao, itakapocheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Timu ya Lipuli ya Iringa.
Imetolewa na.....
HAJI S. MANARA
Mkuu wa Habari na mawasiliano Simba Sports Club.
All the best Ndemla , we love you Simba sc fans,
ReplyDeleteThis is Simba !!
Wamchukue yule banka wa mtibwa azibe nafasi yake asaidiane na mzamiru
ReplyDelete