November 21, 2017



Makamu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura amesema, kuna uwezekano mkubwa Bara la Afrika, likatoa idadi kubwa ya waamuzi katika fainali za michuano mikubwa hususani Kombe la Dunia.

Wambura alisema hayo Jumatatu Novemba 20, 2017 kwenye Ukumbi wa ILO, Dar es Salaam wakati aifungua kozi Wakufunzi wa Waamuzi kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika.

Kozi ya wiki moja ya Wakufunzi wa waamuzi hatua ya tatu ‘Futuro III’ inayofanyika Tanzania kwa nchi 26 kushiriki. Jumla ya Washiriki 58 wanashiriki kozi hiyo kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania.

Kozi hiyo ina wakufunzi sita wakiwamo Carlos Henriques na Dominic Chiellens wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), ambao Wambura aliwataka wakufunzi wanaofundishwa mbinu mbalimbali kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza ndoto hiyo ya Afrika.

“Waamuzi wa Afrika wana uwezo. Ninyi wakufunzi ni wa kufanya waamuzi wetu kuwa na uwezo zaidi. Ni Aibu kwa Bara kubwa kama Afrika lenye nchi wanachama 54 wa FIFA kuwa na waamuzi wachache katika fainali za Kombe la Dunia.


“Tuazimie kuwa na waamuzi wa kutosha katika fainali kubwa kama hizo,” Amesema Wambura ambaye alipigiwa makofu na washiriki kwa kuwatia shime wakufunzi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic