Amissi Tambwe ameendelea na mazoezi ya taratibu akijifufua kutaka kurejea dimbani.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuwa mfungaji bora mara mbili, alionekana akizunguka uwanja wakati wa mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru, leo.
Tambwe anataka kurejea na kuichezea Yanga baada ya kukaa nje licha ya Yanga kucheza mechi 10 za Ligi Kuu Bara.
Mshambuliaji huyo raia wa Burundi, amekuwa majeruhi kwa kipindi chote tokea ligi hiyo ilipoanza mwishoni mwa Agosti.
Wakati Tambwe akiendelea kujifua, beki Kelvin Yondani ambaye ilielezwa kuwa ana majeruhi madogo, naye alianza mazoezi.
Lakini Thabani Kamusoko na Papy Tshishimbi nao walishindwa kufanya mazoezi ikielezwa kwamba bado ni majeruhi.
0 COMMENTS:
Post a Comment