November 22, 2017





Mshambuliaji wa Everton FC, Oumar Niasse amefungiwa kucheza mechi mbili kwa kosa la kujiangusha.

Niasse raia wa Senegal alifanya hivyo wakati timu ikiivaa Crystal Palace na kupata sare ya mabao 2-2 yeye akifunga moja.

Chama cha Soka England (FA) kimepitisha sheri a ya kutoa adhabu kwa wale watakaokuwa wamejiangusha. Baada ya kujiangusha, mwamuzi alitoa penalti na Everton ikafanikiwa kupata bao.

Kama litatokea tukio hilo, litachukuliwa uamuzi hata baada ya mechi.


Hivyo, Niasse anakuwa mchezaji wa kwanza kuadhibiwa Ligi Kuu England baada ya mechi kutokana na tukio la kujiangusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic