Klabu ya Simba imeanza kumpigia chepuo mshambuliaji, Elias Maguri.
Taarifa zinaeleza Maguri aliamua kuondoka nchini Oman alipokuwa anakipiga kwa kuvunja mkataba na sasa ni mchezaji huru.
Lakini kumekuwa na taarifa kwamba kuna ofa nchini Morocco, lakini Yanga tayari imetupa ndoano ikiwezekana kumnasa kuongeza nguvu katika ushambulizi.
Pamoja na hivyo, Simba nao wanaona Maguri anaweza kuwasaidia na kwa kuwa ni mchezaji wao wa zamani wanapanga kumsogelea na kuangalia mambo.
Lakini kuna taarifa Simba wanasubiri ripoti ya mwalimu wao Joseph Omog ili waanze usajili katika dirisha dogo.
Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili ya Simba amesema, wanaamini mwalimu wao atataka mshambuliaji.
"Akitaka mshambuliaji, Maguri tunaona anaweza kuwa msaada. Hivyo tunaweza kufanya naye mazungumzo hivi karibuni ili kuona inakuwaje," alisema.

0 COMMENTS:
Post a Comment