Saimon Msuva ameendelea kuonyesha kuwa yuko vizuri baada ya kufunga bao pekee timu yake ikilala kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Morocco.
Difaa Al Jadida iliyokuwa ugenini, imelala kwa mabao 2-1 dhidi ya vigogo wa nchi hiyo Wydad Casablanca.
Wenyeji walipata penalti katika dakika ya 37, bao lao likifungwa na Khadrouf na likadumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili mapema katika dakika ya 52, Cheick Camara akafunga bao safi la pili na Msuva akajibu kwa kufunga katika dakika ya 65.
Baada ya hapo, Wydad walilazimika kurudi nyuma na Difaa walikuwa wakishambulia kwa kasi kubwa hata hivyo hawakupata bao la kusawazisha.
Msuva aliyetokea Yanga amekuwa akionyesha uwezo mkubwa wa kufunga akiwa na timu yake hiyo mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment