MASHABIKI WA PRISONS YA MBEYA. |
Klabu ya Tanzania Prisons imepewa Onyo Kali kwa kuwakilishwa kwenye benchi na ofisa tofauti na yule aliyeudhuria kikao cha maandalizi (pre match meeting) cha mchezo kati yake na Kagera Sugar uliofanyika Novemba 4, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Uamuzi huo umetoka katika Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa kikao chake siku chache zilizopita.
Pia, mchezaji Benjamin Asukile wa Tanzania Prisons amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu na Mwamuzi kwa kosa la kumpiga kiwiko kwenye paji la uso mchezaji wa Kagera Sugar.
Katika kikao hicho, Prisons iliwakilishwa na Meneja wake Erasto J. Ntabah lakini kwenye benchi alikaa Hassan Mtege. Adhabu ya Onyo Kali kwa klabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Pia Erasto J. Ntabah amesimamishwa hadi suala lake la kutoka jukwaani na kwenda kumfokea Mwamuzi wa Akiba litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Amesimamishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment