November 23, 2017




Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Novemba 22, 2017 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi kwa msimu wa 2017/2018 inayoendelea hivi sasa.


Kwa upande wa Ligi Daraja la KwanzaKlabu ya Mvuvumwa imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi dhidi ya African Lyon ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza. Mechi hiyo ilifanyika Novemba 7, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


Mtunza Vifaa wa timu ya JKT Mlale, Noel Murish amesimamishwa hadi suala lake la kuwamwagia maji washabiki wa Polisi Tanzania litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Uamuzi wa kumsimamisha ni kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Usimamizi wa Ligi. Alifanya kitendo hicho katika mechi hiyo iliyochezwa Novemba 4, 2017 kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic