November 7, 2017



Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amekuwa gumzo kubwa wakati Simba ikiwa safari kwenda Katavi.

Kila sehemu basi la Simba liliposimama, mashabiki wa Simba walikuwa wakipiga kelele kutaka kumuona Kichuya.




Mashabiki hao waliomba kumuona Kichuya na faida yao ilikamilika kila walipomuona.

Umaarufu wa Kichuya umezidi kupanda baada ya kufunga mabao katika mechi mbili mfululizo.


Kichuya alifunga bao katika mechi dhidi ya Yanga wiki iliyopita, mechi ikaisha kwa sare ya bao 1-1 lakini akafunga tena Simba ilipoishinda Mbeya City kwa bao 1-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic