Klabu ya Yanga imechoshwa na tabia ya straika wao, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe kutokana na kwenda kwao huku akishindwa kurejea mpaka jana mchana, hivyo wamepanga kumpa adhabu.
Ngoma ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili utakaomalizika mwaka 2019, aliripotiwa kuwa majeruhi ambapo alirejea kwao na mpaka jana alikuwa hajaripoti kwenye kituo chake cha kazi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Dismas Ten, alisema Ngoma tangu aondoke amekuwa akiwasumbua kutokana na kutotoa ushirikiano kila wanapomtafuta.
Alisema akirejea ni lazima wamuadhibu kwa kuwa muda aliopewa kwa ajili ya kushughulikia matatizo yake umepita na hawajui atarejea lini huku akisisitiza ni lazima arejee kwani wana mkataba naye.
“Ngoma anatusumbua sana kila tunapojaribu kuwasiliana naye amekuwa hatoi ushirikiano wa kutosha, hivyo akirejea lazima tumuadhibu kwani muda aliopewa umemalizika,” alisema Ten.
CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:
Post a Comment