Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Novemba 22, 2017 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi kwa msimu wa 2017/2018 inayoendelea hivi sasa.
Klabu ya Coastal Union imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi ikiwa na maofisa pungufu, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza. Ilifanya hivyo katika mechi dhidi ya JKT Mlale iliyofanyika Novemba 12, 2017 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza. Ilifanya hivyo katika mechi dhidi ya JKT Mlale iliyofanyika Novemba 12, 2017 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Nayo Klabu ya JKT Mlale imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Daraja la Kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment