November 20, 2017

USENGIMANA


Kiungo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, raia wa Uganda, kwa sasa ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Bara, lakini wapinzani wake wameanza kumuwinda kimyakimya wakitaka kumpiku.

Miongoni mwa wanaojipanga kwa ajili ya kumpiku Okwi ni straika wa Singida United, Danny Usengimana na yule wa Prisons, Mohammed Rashid.

Ikumbukwe kuwa, kabla ya mechi za jana Jumapili za ligi hiyo, Okwi alikuwa kileleni mwa ufungaji akiwa na mabao nane, akifuatiwa na Mohammed Rashid wa Prisons aliyefunga mabao sita.

Usengimana alisema: “Nahitaji kuwa bora kila siku, ili kufanikisha hilo, nimekuwa nikifanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha nafikia malengo niliyojiwekea.

“Nimejipanga kweli kuona naendelea kufunga mabao kadiri niwezavyo, lengo likiwa ni kumaliza msimu nikiwa kinara na kuibuka na tuzo ya ufungaji bila ya kujali ushindani uliopo sasa.”


Naye Rashid alisema: “Nitafurahi kama nikiibuka kuwa mfungaji bora msimu huu, kuwa nyuma ya kinara kwa mabao mawili wala hainipi shida sana, nitaendelea kupambana kuhakikisha nafikia malengo yangu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic