November 20, 2017



Kikosi cha Lipili FC ya Iringa kipo katika mazungumzo ya  mwisho kwa ajili ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Yanga, Anthony Matheo, wanayemtaka kwa mkopo.

Timu hiyo, inamtaka mshambuliaji huyo kwa ajili ya kuiimarisha safu ya ushambuliaji wa timu hiyo inayoongozwa na Malimi Busungu na Salum Machaku.

Matheo hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha Mzambia, George Lwandamina kutokana na ushindani uliopo katika timu hiyo.

Kocha wa Lipuli, Selemani Matola alisema timu yao ina upungufu kwenye safu ya ushambuliaji ambayo inahitaji kuboreshwa katika usajili huu wa dirisha dogo.

Matola alisema, wapo kwenye mazungumzo mazuri na Yanga baada ya kufikia muafaka mzuri wa kukamilisha dili hilo.

“Matheo ni kati ya washambuliaji waliopo kwenye mipango yetu ya usajili katika dirisha dogo lililofunguliwa wiki iliyopita.

“Tunataka kumsajili Matheo kwa ajili ya kuiboresha safu yangu ya ushambuliaji ambayo ndiyo nimeiona inahitaji kufanyiwa marekebisho.

“Ninaamini kama nikifanikiwa kumpata Matheo nitakuwa nimekamilisha usajili wangu katika usajili huu kwani tayari tupo katika muafaka mzuri wa kuwapata washambuliaji wa Simba, Liuzio (Juma) na Mnyate (Jamal),” alisema Matola.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic