November 19, 2017


Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga inaibuka na ushindi wa mabao 5-0.


Dk ya 93: Muda wowote kuanzia sasa mchezo utamalizika.

Dk ya 90: Shangwe zinaongezeka kwa Yanga, mwamuzi wa akiba anaonya dakika 3 za nyongeza.

Dk ya 86: Yanga wanaongeza kasi, mashabiki wao wanashangilia kwa nguvu zaidi.

Dk ya 80: Yanga wanapata bao la tano, kazi nzuri ya Gadiel Michael anampa pasi Martine ambaye anafunga bao la kwa shuti.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 74: Mashabiki wa Mbeya City wanaonekana kutoamini kinachotokea, wamepunguza kasi ya kushangilia.

Dk ya 68: Mrisho Ngassa anatoka, anaingia Victor Hangaya.

Dk ya 59: Chirwa anaipatia Yanga bao la nne akimalizia pasi ya Ibrahim Ajibu.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 57: Mbeya City wanafika langoni mwa Yanga lakini wanakuwa wameotea.

Dk ya 54: Yanga wanaendeleza kucheza kwa kasi.

Chirwa anapiga penalti nzuri, inajaa wavuni.

Dk ya 50: Gooooooooooooooooooo

Kipa wa Mbeya City anapata kadi ya njano kwa kumuangusha Raphael Daudi ndani ya eneo la 18.

Dk ya 48: Yanga wanapate penalti.

Kipindi cha pili kimeanza.

MAPUMZIKO

Dk ya 49: Kipindi cha kwanza kimekamilika. Yanga iko mbele kwa mabao 2-0.

Dk ya 45: Zinaongezwa dakika 4, Martine wa Yanga ameumia, yupo chini.

Dk ya 44: Mbeya City wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa.

Dk ya 42: Buswita anachezewa faulo na Mwasapili ambaye anapewa kadi ya njano.

Dk ya 39: Mbeya City wanapata kona. Inapigwa kona fupi, inatoka nje.

Dk ya 34: Juma Abdul wa Yanga anapata nafasi ya kufika langoni mwa Mbeya City lakini shuti lake linatoka nje.

Dk ya 30: Emmanuel Martine wa Yanga anapewa kadi ya njano kwa kiucheza faulo.

Dk ya 30: Yanga wanakosa nafasi ya wazi kabisa, Buswita anabaki na kipa anashindwa kufunga.

Dk ya 29: Mrisho Ngassa wa Azam anajaribu kupambana lakini mambo yanakuwa magumu.

Dk ya 23: Yanga wanapata bao la pili kupitia kwa Emmanuel Martine ambaye aliwatoka walinzi wa Mbeya City na kufunga.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 22: Yanga wameanza kutulia.


Beki wa Mbeya City Mkandawile anapewa kadi ya njano kwa kumlalamikia mwamuzi kiasi cha kumshika bega kuhusu bao la Chirwa.

Dk ya 20: Chirwa anaipatia Yanga bao la kwanza kutokana na uzembe wa walinzi.

Goooooooooooooooooooooooo

Dk 16: Obrey Chirwa anaumia, mchezo umesimama kwa dakika mbili atibiwe, kisha unaendelea.

Dk ya 15: Mbeya City wanapata faulo nje kidogo ya 18 ya Yanga lakini shuti linapaa juu ya lango.

Dk ya 12: Lundenga wa Mbeya City yupo chini ameumia, mchezo unasimama kwa muda. 

Dk ya 10: Yanga wanamili mpira muda mwingi sasa.
Dk ya 8: Chirwa anaingia na mpira lakini walinzi wanamuwahi.

Dk ya 7: Mbeya City wanaonekana kujipanga na kutengeneza nafasi.

Dk ya 3:  Timu zote zinaongeza kasi pia.

Dk ya 2: Yanga wanaongeza kasi taratibu.

Mchezo umeanza. Mashabiki siyo wengi kama ilivyokawaida pindi kunapokuwa na mchezo mkubwa.

Timu zimeingia uwanjani.


Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, unachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic