December 15, 2017



Kocha wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, John Mwansasu ameita wachezaji 16 watakaoingia kambini kesho Jumamosi Desemba 16, 2017 kujiandaa na michuano ya Copa Dar es Salaam itakayofanyika kwa siku mbili kwenye Ufukwe wa Coco.
Kikosi hicho cha wachezaji 16 kitaingia kambini kwa muda wa wiki nzima kujiandaa na mashindano hayo ya kimataifa yatakayojumuisha timu nne ambazo ni Malawi, Uganda, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara.

Wachezaji walioitwa ni pamoja na Rajabu Ghana (Huru), Khalifa Mgaya (Chuo cha CBE), Juma Kaseja (Kagera Sugar), Juma Sultan (Chuo Kikuu Ardhi), Ally Rabby (Huru), Mwalimu Akida (Huru), Samwel Salonge (Huru), Athuman Idd 'Chuji' (Coastal Union), Kenan Mwandisi (Huru).

Wengine ni John Pauseke (Huru), Joseph Jafet (Huru), Jaruph Rajab Juma (Chuo cha DIT), Mbwana Mshindo (Chuo cha DSJ), Rolland Msonjo (Singida United), Jerry Francis Robert (Huru) na Haruna Moshi (Friends Rangers)

Benchi la ufundi linaongozwa na Mwansasu mwenyewe akisaidiwa na kocha wa makipa Peter Manyika, Meneja Deo Lucas na daktari wa timu Richard Yomba.


Kocha John Mwansasu amesema mashindano hayo ya Copa Dar Es Salaam yatakayofanyika Desemba 25 na 26, 2017 yatasaidia kuwaongezea uzoefu zaidi kwa mchezo huo wa soka la Ufukweni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic