December 20, 2017



Zoezi la kuwakabidhi washindi wa promosheni ya Shinda na SportPesa linaendelea na hivi karibuni  mwakilishi wa SportPesa Frank Charles Gibebe  aliwasili Buzurugwa Nyakato ambapo alikabidhi bajaji aina ya TVS King Deluxe ya Michael Gogah (33) aliyeibuka mshindi wa droo ya 31 iliyofanyika tarehe 25 Novemba. 

Makabidhiano hayo yalifanyika nyumbani kwa dada wa mshindi bi. Samia Gogah, aliyekabidhiwa kwa niaba ya mshindi Michael ambaye alikuwepo Nairobi Kenya kwa shughuli za kibiashara. 

Ndugu hao wanaojishughulisha na biashara za kuuza rejeta, wameishukuru kampuni ya Sportpesa kwa promosheni hiyo ambayo kwa sasa inaenda kumsaidia mshindi katika shughuli zake binafsi na pia katika kumuingizia kipato cha ziada. 

"Nimehamasika sana, maana siku ile aliyonipigia kunifahamisha kuwa ameshinda, na mimi kinajiunga na SportPesa. Ninawaambia Watanzania washiriki SportPesa kwani mshindi ni halali kabisa na ni mdogo wangu " alisema bi Samia Gogah.


"Tunaendelea kuwaneemesha Watanzania hususani wale wanaopenda kubadilisha maisha yao. TVS King Deluxe zipo nyingi na zinasubiri Watanzania wazinyakue kila siku.

Ili kushiriki katika promosheni ya Shinda na SportPesa, mteja atalazimika kutuma neno GAME kwenda 15888 ili kujisajili, kisha atafuata maelekezo yatakayokuja kwa njia ya ujumbe. Mteja atakeyeweka ubashiri kwa njia yoyote ile anashauriwa kutuma neno SHINDA kwenda 15888 mara baada ya kuweka huo ubashiri ili aweze kuingia kwenye droo ya kujishindia bajaji hizi" alisema Meneja Uhusiano na Mawasiliano SportPesa, Adventina Kiyeyeu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic