December 20, 2017



Uongozi wa klabu ya Simba umeandika barua kwenda Lipuli ukiiomba klabu hiyo kuiachia imuachie.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ambaye amerejea nchini, amelifafanua jambo hilo la beki Asante Kwasi ambaye kumekuwa na mvutano kati ya Simba na Lipuli kuhusiana na yeye kuhamia Msimbazi.

“Suala la Kwasi nimelikuta na Simba tunamhitaji kweli, tumeandika barua kwa Lipuli na tunasubiri vizuri,” alisema Hans Poppe.

“Hakukuwa na tatizo, tulikwenda kuangalia mikataba yake na Kwasi anamilikiwa na akademi na yuko chini ya ajenti wake. Tulichoangalia kwanza kama anaweza kupatikana na tukafanya mawasiliano na ajenti wake.

“Sasa wakati tunafanya mazungumzo na ajenti wake, ndiyo kukawa na maneno kwamba mambo yanakwenda kinyemela. Lakini Kwasi kama atakuja Simba basi atatua kwa kufuata utaratibu unaotakiwa,” aliongeza.

“Unajua Kwasi ana mkataba na akademi, ana mkataba na Lipuli na mkataba na ajenti wake. Hivyo ni lazima tumalizane na wote tena kwa kufuata utaratibu.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic