December 27, 2017



Kampuni ya kutengeneza vifaa ya Macron ambayo imeingia mkataba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kutengeneza jezi na vifaa kwa ajili ya timu za taifa.

Macron ni kampuni kutoka nchini Italia na inatumika na timu nyingi maarufu kwa upande wa klabu zikiwemo timu za taifa za nchi.

Pamoja na kutumiwa na zaidi ya nchi zaidi ya 60, Macron pia inatumika katika timu maarufu za Italia na England.

Timu za Italia zinazotumia jezi za Macron ni pamoja Lazio, Bologna, Cagliari, Spal zote zinashiriki Serie A. Pia kuna timu kutoka Ureno kama Sporting Lisbon, Nice ya Ufaransa ambayo anaitumikia Mario Balotelli lakini Clube Brugge ya Ubelgiji.


Kuna timu kama Dinamo Bucarest ya Romania, Red Stars ya Serbia kwa England ni Stoke City na Albania ni kati ya timu za taifa zinazotumia uzi huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic