Uongozi wa klabu ya Lipuli FC umethibitisha kupokea barua kutoka Simba inayomtaka beki Asante Kwasi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema wamepeleka barua kwa Lipuli FC baada ya kugundua bado ana mkataba na klabu hiyo pamoja na wakala wake pia.
Lakini leo, Lipuli FC kupitia taarifa katika klabu yao wamesema wamepokea barua na wanaikaribisha Simba mezani.
“Tayari tumepokea barua yao, wanamhitaji Kwasi na sisi hatuna shida, tunawakaribisha mezani.”
0 COMMENTS:
Post a Comment