Simba imefanikiwa kumsajili mshambuliaji mpya aitwaye Antonio Dayo Domingues.
Domingues anatokea nchini Msumbiji na taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza anachukua nafasi ya Laudit Mavugo, raia wa Burundi.
Mshambuliaji huyo kinda anasifika kwa kuwa na kasi na mashuti makali, amesaini miaka miwili tayari kuanza kuitumikia Simba na tayari ametua nchini kikazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment