December 23, 2017




Mwanachama maarufu wa Simba, Mohamed Dewji maarufu kama Mo, amemtaka Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog kujiuzulu.


Mo Deji kupitia mtandao ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Twitter amemtaka Omog kujiuzulu baada ya Simba kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Shirikisho jana na timu ya daraja la pili ya Green Worriers.

Dewji amesema hana uamuzi kwa kuwa kama mwanachama wa kawaida anamuomba au kumshauri Omog kuachia ngazi.

Mo Dewji ndiye aliyeshinda nafasi ya uwekezaji katika klabu ya Simba inagawa suala hilo bado halijakamilika na yeye akaanza kazi rasmi.

Simba imeng'olewa katika michuano hiyo na Green Worriers ambayo inashiriki Ligi Daraja la Pili baada ya kumaliza dakika 90 kwa bao 1-1 Simba wakisawazisha na mikwaju ya pexnalti wakatwangwa 4-3.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic